Monday, April 18, 2016

BIMA KUTOA ELIMU YA AFYA KWA WANAMUZIKI WA INJILI TANZANIA IKIAMBATANA NA TAMASHA LA MAOMBI NA KUSIFU

Chama cha Muzikiwa Injili Tanzania (CHAMUITA)  kinawatangazia wanamuziki wote wa Injili na wadau nchinmi Tanzania  kuwa tarehe 30.04.2016 kutakuwa na kongamano la CHAMUITA ambalo watu wa BIMA ya afya NHIF watakuwepo kutoa elimu kuhusu umuhimu na faida za wanamuziki kujiunga na mfuko huo wa Taifa wa BIMA ya Afya kwa gharama nafuu kupitia CHAMUITA kwaajili ya kupeana taarifa na mikakati mbalimbali pamoja na kuzipanga zile kamati za CHAMUITA kiutendaji ili kila mmoja ajue kamati yake na kwamba anawajibika kwa nani.
Katibu Muenezi wa Chama Cha Muziki wa Injili Tanzania, Stella Joel

Pia kutakuwa na uimbaji siku hiyo pamoja na maombi yetu ya kawaida. Kongamano litaanza asubuhi mpaka baadae. Tunategemea kuwa na wageni mbalimba siku hiyo. Event nzima itafanyikia katika kanisa la Right House, na kama kutakuwa na mabadiliko utayapata kupitia blogu hii.

Wale wenye kadi na vitambulisho vya BIMA mnaombwa sana kuja navyo ni muhimu sana. BIMA ya Afya imetoa gharama nafuu kwa wanamuziki wa Injili Tanzania kwa kuchangia Tshs. 76,800 tu kwa mwaka badala ya Tshs. 900,000. Mungu akubariki sana.

TUMAINI NJOLE AFANYA MAAJABU KATIKA IBADA YA JUMAPILI 17.04.2016 KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" WENGI WASHANGAZWA

Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Tanzania Tumaini Njole aliyealikwa katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" Assemblies of God linaloongozwa na Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliweza kufanya vitu ambavyo watu hawakutegemea kuona mwimbaji wa nyimbo za Injili ana nguvu za MUNGU kiasi hicho. Wengi watokwa na machozi huku wakimsikiliza vile ambavyo tunaamini Mungu alikuwa akimuongoza afanye. Ungana nami kuangalia clip hii

Friday, April 8, 2016

VITAMBULISHO VILIVYOTOKA NA KUKABIDHIWA NA KATIBU MUENEZI STELLA JOEL KUTOKA RUMAFRICA TAREHE

 Hawa ni wanachama halali walitimiza sheria zote za kuwa wanacahama wa Chama Cha Muziki wa Injili Tanzania, na wana haki wa kupata haki zao zote kutoka katika chama hiki. Unakaribihwa sana wewe mwimbaji na mwanamuziki yeyote wa Gospel kujiunga na chama hiki. Nafasi zipo wazi.










MWANACHAMA WA CHAMUITA MC. JOSHUA MAKONDEKO AMSHUKURU MHE. GODBLESS LEMA

Mc. Joshua Makondeko anayetamba kwa kibao cha Tutapita Katikati yao alikuwa na haya ya kusema kwa familia ya Mh. Godbless Lema "Asanteni sana FamiLia ya Mbunge wa Arusha Mjini Mhe. GodbLess Lema Kwa Kuniamini na Kunipa Kazi ya Kusherehesha SendOffParty ya Mtoto Wenu EmMy Lema. 
Ndani ya Mwika Ilikuwa ni Shamrashamra na Nderemo. 
Asante sana. .hezron Tz, christopha Mhangila, Smrt boy Emanuel Peter,Kennedy Daudi na Alfredy Funda kwa Kuja Kunipa Kompani. 
ALl the best EmEns. 










Friday, April 1, 2016

UONGOZI WA CHAMUITA UNAKUOMBA KUKAMILISHA VILE VINAVYOHITAJIKA KATIKA VITAMBULISHO VIPYA VYA CHAMUITA 2016-2020

Uongozi wa CHAMUITA unakuomba wewe mwimbaji wa njyimbo za Injili Tanzania ambaye umejiunga na Chama Cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA) ambaye hujakamilisha na hujapata kitambulisho chako kipya cha mwaka 2016-2020, unaombwa kukamilisha taarifa zako na tuma kwa Katibu Muenezi CHAMUITA da Stella Joel, namba yake ipo kwenye kitambulisho hapo chini.
Tunachotaka kutoka kwako ni
1. Jina lako kamili
2. Mahali unapoishi au Box
3. Saini yako
4. Namba ya simu
5. Nafasi yako au cheo chako CHAMUITA

Mfano wa kitambulisho



WANA-CHAMUITA WAZIDI KUSHIRIKI KATIKA MATAMSHA MBALIMBALI, JUMAPILI HII WATAKUWEPO MSASANI KKKT KWENYE UZINDUZI WA DVD YA ATUPYANIE PAULO


WALIOTEMBELEA - VISITORS

BLOG designer: Rumafrica

BLOG designer: Rumafrica
Blog hii imetegenezwa na Rumafrica +255 715 851 523 | www.rumaafrica.blogspot.com | www.facebook.com/Rulea Sangaa/