Monday, April 18, 2016

BIMA KUTOA ELIMU YA AFYA KWA WANAMUZIKI WA INJILI TANZANIA IKIAMBATANA NA TAMASHA LA MAOMBI NA KUSIFU

Chama cha Muzikiwa Injili Tanzania (CHAMUITA)  kinawatangazia wanamuziki wote wa Injili na wadau nchinmi Tanzania  kuwa tarehe 30.04.2016 kutakuwa na kongamano la CHAMUITA ambalo watu wa BIMA ya afya NHIF watakuwepo kutoa elimu kuhusu umuhimu na faida za wanamuziki kujiunga na mfuko huo wa Taifa wa BIMA ya Afya kwa gharama nafuu kupitia CHAMUITA kwaajili ya kupeana taarifa na mikakati mbalimbali pamoja na kuzipanga zile kamati za CHAMUITA kiutendaji ili kila mmoja ajue kamati yake na kwamba anawajibika kwa nani.
Katibu Muenezi wa Chama Cha Muziki wa Injili Tanzania, Stella Joel

Pia kutakuwa na uimbaji siku hiyo pamoja na maombi yetu ya kawaida. Kongamano litaanza asubuhi mpaka baadae. Tunategemea kuwa na wageni mbalimba siku hiyo. Event nzima itafanyikia katika kanisa la Right House, na kama kutakuwa na mabadiliko utayapata kupitia blogu hii.

Wale wenye kadi na vitambulisho vya BIMA mnaombwa sana kuja navyo ni muhimu sana. BIMA ya Afya imetoa gharama nafuu kwa wanamuziki wa Injili Tanzania kwa kuchangia Tshs. 76,800 tu kwa mwaka badala ya Tshs. 900,000. Mungu akubariki sana.

No comments:

Post a Comment

WALIOTEMBELEA - VISITORS

BLOG designer: Rumafrica

BLOG designer: Rumafrica
Blog hii imetegenezwa na Rumafrica +255 715 851 523 | www.rumaafrica.blogspot.com | www.facebook.com/Rulea Sangaa/