Wednesday, March 30, 2016

PICHA ZA TAMASHA LA CHAMUITA SIKU YA PASAKA ARUSHA 27.03.2016

CHAMUITA ARUSHA inamshukuru sana Mungu kwa kuweza kufanya tamasha kubwa ambalo limeweka historia kwa mwaka 2016 katika jiji la Arusha. Ilikuwa si rahisi ila kwa msaada wa Mungu tamasha liliweza kufanyika kwa mwitikio mkubwa sana, na kila aliyefika mahali hapo aliweza kubarikiwa kwa Neno na uimbaji kutoka kwa waimbaji waliochini ya CHAMUITA. Hakika tuliuona mkono wa Bwana ukitembea kwa watu wake.

Lengo la tamasha hili ni kutangaza CHAMUITA kwa wakazi wa Arusha na dunia nzima kwa kupitia mitandao na media mbalimbali. Katika tamasha hili kulikuwa na kwaya nne, vikundi vitatu vya Praise and Worship, madhehebu mbalimbali, maaskofu wawili, wachungaji saba.

Katika tamasha hili tuliweza kupata kondoo wapya waliamua kujiunga na chama hiki na wakaweza kuchukua fomu za kujisajili. Na hii inaonyesha ni namna gani Mungu wetu amekikubali chama hiki kuwa ni chombo chake cha kutumia kufikisha ujumbe kwa watu kupitia vinywa vya waimbaji. 

Chama Cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA) kwa kanda ya Arusha kilizindiliwa rasmi 10.10.2015 katika kanisa la Maranatha Arusha. Mpaka dakikia hii kina wanachama wasiopungua 150. Rais wa Chama hiki kwa Tanzania nzima ni Nabii Mwanasheria Dr. Addo November na pia ni mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania. Tuone sasa matukio katika picha





UKITAKA KUONA MATUKIO ZAIDI YA TAMASHA HILI BONYEZA "READ MORE" HAPO CHINI KIDOGO KULIA

TUZIDI KUWAOMBEA ROSE MUHANDO NA ALEX MSAMA KWANI WAZIRI NAPE ANATAKA "FAILI" LA ROSE MUHANDO KUTOSHIRIKI TAMASHA LA PASAKA MWANZA

Jamani Rose Muhando na Msama ni ndugu zetu waliomo katika Chama Cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA) hivi karibuni wamekubwa na hili tatizo la mmojawapo kutoshiriki tamasha la Pasaka Mwanza kama inavyoelezwa hapo chini.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye

Na Idd Mumba, RISASI Mchanganyiko
MWANZA: Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametaka kupewa maelezo maalum ya kimaandishi juu ya mwenendo wa mwimbaji wa nyimbo za Injili, Rose Muhando ili aweze kuchunguza madai ya utapeli yanayosemwa juu yake.

Nape alitoa kauli hiyo baada ya kuulizwa endapo atafanyia kazi tuhuma zilizotolewa na waandaaji wa Tamasha la Pasaka la kila mwaka, Msama Promotions, waliodai mwimbaji huyo hakutokea jukwaani, licha ya kupewa malipo yake na stahiki zingine zilizostahili.

Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Rose Muhando.

“Kwanza ieleweke kuwa mimi sikuambiwa, ila nilisikia wakiwatangazia watu waliokuwepo uwanjani juu ya kutokuwepo kwa Rose kwenye tamasha hilo. Sasa mimi siwezi kufanya kazi kwa maneno ya mtaani, kama kuna wasanii wanatapeli, niletewe maelezo kimaandishi yakiwa na ushahidi wa tuhuma zao, hapo ndipo nitaweza kujua hatua za kuchukua,” alisema.

Awali, ofisa mmoja wa Msama Promotions aliyeomba hifadhi ya jina lake kwa kuwa siyo msemaji, alisema Rose alikuwa amepewa malipo yote, ikiwa ni pamoja na usafiri wa gari la kumtoa Dodoma hadi Mwanza, lakini hakuweza kutokea katika onesho hilo.

“Tulishamalizana na Rose na kila mmoja alijua atakuwepo, lakini tunashangaa mara ya mwisho hapatikani kwenye simu na hatujui kapatwa na masaibu gani,” alisema ofisa huyo.
Gazeti hili lilijaribu kumtafuta mwimbaji huyo nyota ili atoe ufafanuzi wa madai hayo, lakini simu yake ya mkononi haikupatikana. Rose Muhando ni miongoni mwa wasanii ambao wanasimamiwa na Alex Msama, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo.

LEO TUBARIKIWE NA WIMBO WA MADAM RUTI WA AMENIBAMBA…KARIBUNI

Tuesday, March 29, 2016

MWANACHAMA WA CHAMUITA MC. JOSHUA MAKONDEKO AKONGA MIYO YA WATU NDANI YA MEGA MKATE NA PRAISE POWER RADIO URAFIKI SOCIAL HALL JIJINI DAR ES SALAAM

MC. Joshua Makondeko ni mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania, Mtangazaji wa LTV Tanzania na pia ni Mwanachama wa Chama Cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA). Siku ya Jumapili ya Pasaka 27.03.2016 aliweza kufanya vizuri sana katika tamasha la Mega Mkate na Praise Power Radio lililofanyika katika ukumbi wa Urafiki Social Hall Sinza Legho jijini Dar es Salaam.

Monday, March 28, 2016

MLEZI WA CHAMA CHA MUZIKI WA INJILI TANZANIA ALEX M. MSAMA AFANYA TAMASHA LAKE LA PASAKA CCM KILUMBA JIJINI MWANZA KWA KISHINDO NA GOODLUCK GOZBERT AZINDUA ALBAM YAKE

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye (pichani chini) akizindua rasmi albam mpya ya mwimbaji Goodluck wakati wa tamasha la Pasaka lililofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Mwanza , Wabunge pamoja na Maaskofu wa makanisa ya Mwanza.

Tamasha hilo ambalo limehudhuriwa na mashabiki wengi mkoani humo limetumbuizwa na waimbaji mbalimbali wa nyimbo za injili kutoka hapa nchini na nchi jirani za Zambia na Kenya, waimbaji hao ni Upendo Nkone , Martha baraka , Jesca BM, Joshua Mlelwa , Tumsifu Rufutu, Christopher Mwahangila, Jeniffer Mgendi, Bonny Mwaiteje, Goodluck ambaye amezindua albam yake mpya na waimbaji Faustine Munishi kutoka nchini Kenya, Solomon Mukubwa kutoka Nchini Kenya pamoja na Ephraim Sekereti kutoka nchini Zambia wote kwa pamoja wamefanya maonesha mazuri yaliyopagawisha mashabiki wa muziki wa injili katika uwanja wa CCM Kirumba na kuwafanya wacheze kila wakati, katika picha kulia ni mwimbaji Goodluck na kushoto ni Bw. Alex Msama Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion inayoandaa matamasha hayo.

Tamasha hilo litaendelea kesho kwa onesho kabambe linalotarajiwa kufanyika mjini Kahama mkoani Shinyanga baada ya kumaliza maonyesho mawili katika mikoa ya Geita na Mwanza.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-MWANZA)

Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye wa nne kutoka kulia akimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. John Mongela alipokuwa akimkaribisha rasmi ili kutoa salam zake kutoka kwa serikali.

Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akishiriki katika sala maalum ya kuombea albam ya mwimbaji Goodluck wa pili kutoka kulia iliyotolewa na maaskofu wa Mwanza kabla ya kuizindua.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akishuka kutoka jukwaani kwa ajili ya kuizindua rasmi albam hiyo na kutoa salaam za serikali katika tamasha la Pasaka.

BONYEZA "READ MORE" HAPO CHINI KIDOGO KUONA MATUKIO MENGINE YA TAMASHA HILI

BAADHI YA WANACHAMA WA CHAMA CHA MUZIKI WA INJILI TANZANIA WALIVYOSHIRIKI TAMASHA LA MEGA MKATE NA PRAISE POWER SIKU YA PASAKA 2016 URAFIKI SOCIAL HALL SINZA LEGHO

Hatimaye event ya Mega Mkate na Praise Power Radio imefanyika salama siku ya Pasaka 27.03.2016 katika ukumbi wa Urafiki Social Hall Sinza Legho jijini Dar es Salaam.

Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kufanikisha event hii kufanyika salama. Hakika Mungu alikuwa upande wa Mega Mkate kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Katika event hii tumeona Mungu akiwagusa watu kwa njia ya uimbaji na ujumbe wake aliouweka kwa Mch. Harris Kapiga. Kupitia Mchungaji Harris Kapiga watu tumetoka na fikra zingine na imani yetu imeongezeka na hamu ya kumtumikia Mungu imeongezeka.


Event hii ilikuwa na mvuto wa namna yake na pia kulikuwa na nguvu za Mungu zilizotandaa katika ukumbi huo. Watu wa Mungu waliweza kufurahi na waimbaji mbalimbali waliofika kumtukuza Mungu.

Waimbaji maarufu sana Tanzania kama Bahati Bukuku, Flora Mbasha, Madam Ruti, Andrew Kihwelo, Peaceking David kutoka Nigeria, Edson Mwasabwite, Elizabeth, Mc. Joshua Makondeko, Mess jacob Chengula, Tumaini Njole na wengine wengi waliweza kutuburudisha na kuwakilisha ujumbe wake kupitia vinywa vyao. Hakika watu tulipona Kiroho na kubarikiwa.

Tunamshukuru Bishop Dr. Gertrude Rwakatare Mkurugenzi wa Praise Power Radio na kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa kuiombea event hii na maombi yao tumeona yakifanya kazi na matunda yake tumeona katika Mega Mkate na Praise Power Radio. Mungu azidi kuwabariki na wazidi kuiombea Praise Power Radio kuanzia vyombo, watangazaji na wasikilizaji wazidi kudumu katika kumtafuta Mungu kupitia mafundisho yanayorushwa na radio hii.

Katika even hii watu walioneka kufarijika na kubarikiwa na uimbaji na zoezi zima la kumega mkate ambapo watangazaji waliweza kugawa keki kwa watu wote walioweza kufika katika event hii, na kila mtu aliweza kula keki hiyo.


 MC. Joshua Makondeko - TutapitaKatikatiYao
 Bahati Bukuku
 Flora Mbasha (kushoto)
 Edson Mwasabwite



 Tumaini Njole

 Mtangazaji wa Sifa Moto Praise Power Radio Judith Njole (kushoto) na Madam Ruti (kulia)

 Mess Jacob Chengula


 Mkate wa Mega Mkate na Praise Power Radio

Watangazaji wa Praise Power Radio Frida (kulia) na Victoria Syaona

BONYEZA "READ MORE" HAPO CHINI KUSHOTO KUONA MATUKIO MENGINE YA EVENT HII YA MEGA MKATE

Sunday, March 20, 2016

MATUKIO YA HAFLA YA KUTOA SHAHADA ZA HESHIMA KWA WATUMISHI MBALIMBALI KUTOKA CHUO KIKUU CHA AFRICA GRADUATE UNIVERSITY ILIYOFANYIKA ARUSHA


WAINJILISTI WATUNUKIWA SHAHADA KWA JUHUDI ZAO KATIKA KUHUDUMIA JAMII  



Jumamosi tarehe 19 ndani ya Jiji la Arusha, ilifanyika hafla ya kutoa shahada za heshima kwa watumishi mbalimbali katika kueneza injili ya Yesu, ambapo shahada za aina mbalimbali zimetolewa katika fani ambazo watu hao wapo.

Tukio hilo ambalo limefanywa na Chuo Kikuu cha Afrika chenye makao yake makuu nchini Sierra Leone, kimekabidhi shahada za uzamivu, shahada za uzamili, na pia shahada ya kwanza kwenye tasnia za; Mawasiliano ya Umma, Thiolojia, Usimamizi wa Biashara, Utawala, na kadha wa kadha.

Baadhi ya watumishi waliotunukiwa shahada ni pamoja na Philemon Mollel kutoka Arusha, Chief Prophet Suguye kutoka World Reconciliation Ministries, DSM; Upendo JBride, Stella Joel, Mch. Lucy Wilson, Nabii Okoa Gamba, Nabii Machibya  na wengineo wengi.

Blogu ya Gospel Kitaa iliweka kambi hoteli ya Naura Spring, na zifuatazo ni picha kadhaa za tukio hilo la kihistoria.



Philemon Mollel kutoka Arusha akiwa na Professa Kazembe kutoka Zambia




Chief Prophet Nicholaus Suguye
































Dakta wa Theolojia
Dakta Upendo JBride

WALIOTEMBELEA - VISITORS

BLOG designer: Rumafrica

BLOG designer: Rumafrica
Blog hii imetegenezwa na Rumafrica +255 715 851 523 | www.rumaafrica.blogspot.com | www.facebook.com/Rulea Sangaa/