WAINJILISTI WATUNUKIWA SHAHADA KWA JUHUDI ZAO KATIKA KUHUDUMIA JAMII
Jumamosi tarehe 19 ndani ya Jiji la Arusha, ilifanyika hafla ya kutoa shahada za heshima kwa watumishi mbalimbali katika kueneza injili ya Yesu, ambapo shahada za aina mbalimbali zimetolewa katika fani ambazo watu hao wapo.
Tukio hilo ambalo limefanywa na Chuo Kikuu cha Afrika chenye makao yake makuu nchini Sierra Leone, kimekabidhi shahada za uzamivu, shahada za uzamili, na pia shahada ya kwanza kwenye tasnia za; Mawasiliano ya Umma, Thiolojia, Usimamizi wa Biashara, Utawala, na kadha wa kadha.
Baadhi ya watumishi waliotunukiwa shahada ni pamoja na Philemon Mollel kutoka Arusha, Chief Prophet Suguye kutoka World Reconciliation Ministries, DSM; Upendo JBride, Stella Joel, Mch. Lucy Wilson, Nabii Okoa Gamba, Nabii Machibya na wengineo wengi.
Blogu ya Gospel Kitaa iliweka kambi hoteli ya Naura Spring, na zifuatazo ni picha kadhaa za tukio hilo la kihistoria.
Philemon Mollel kutoka Arusha akiwa na Professa Kazembe kutoka Zambia
No comments:
Post a Comment