Ukiona mtu amekualika katika shughuli yake basi ujue kuna kitu amekiona ndani yako na anatambua mchango wake. Mega Mkate na Praise Power wameona karama aliyonayo mwana CHAMUITA Mc. Joshua Makondeko na wakaamua kumualika akafanye huduma pamoja nao. Sasa kama Mwana CHAMUITA naomba umuombee huyu mtumishi atakapoingia tu ukumbini watu wakapone na kufunguliwa hata kabla ya kuimba. Iombee huduma yake isonge mbele. Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki MC. Joshua Makondeko. Amen
No comments:
Post a Comment