Monday, March 28, 2016

BAADHI YA WANACHAMA WA CHAMA CHA MUZIKI WA INJILI TANZANIA WALIVYOSHIRIKI TAMASHA LA MEGA MKATE NA PRAISE POWER SIKU YA PASAKA 2016 URAFIKI SOCIAL HALL SINZA LEGHO

Hatimaye event ya Mega Mkate na Praise Power Radio imefanyika salama siku ya Pasaka 27.03.2016 katika ukumbi wa Urafiki Social Hall Sinza Legho jijini Dar es Salaam.

Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kufanikisha event hii kufanyika salama. Hakika Mungu alikuwa upande wa Mega Mkate kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Katika event hii tumeona Mungu akiwagusa watu kwa njia ya uimbaji na ujumbe wake aliouweka kwa Mch. Harris Kapiga. Kupitia Mchungaji Harris Kapiga watu tumetoka na fikra zingine na imani yetu imeongezeka na hamu ya kumtumikia Mungu imeongezeka.


Event hii ilikuwa na mvuto wa namna yake na pia kulikuwa na nguvu za Mungu zilizotandaa katika ukumbi huo. Watu wa Mungu waliweza kufurahi na waimbaji mbalimbali waliofika kumtukuza Mungu.

Waimbaji maarufu sana Tanzania kama Bahati Bukuku, Flora Mbasha, Madam Ruti, Andrew Kihwelo, Peaceking David kutoka Nigeria, Edson Mwasabwite, Elizabeth, Mc. Joshua Makondeko, Mess jacob Chengula, Tumaini Njole na wengine wengi waliweza kutuburudisha na kuwakilisha ujumbe wake kupitia vinywa vyao. Hakika watu tulipona Kiroho na kubarikiwa.

Tunamshukuru Bishop Dr. Gertrude Rwakatare Mkurugenzi wa Praise Power Radio na kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa kuiombea event hii na maombi yao tumeona yakifanya kazi na matunda yake tumeona katika Mega Mkate na Praise Power Radio. Mungu azidi kuwabariki na wazidi kuiombea Praise Power Radio kuanzia vyombo, watangazaji na wasikilizaji wazidi kudumu katika kumtafuta Mungu kupitia mafundisho yanayorushwa na radio hii.

Katika even hii watu walioneka kufarijika na kubarikiwa na uimbaji na zoezi zima la kumega mkate ambapo watangazaji waliweza kugawa keki kwa watu wote walioweza kufika katika event hii, na kila mtu aliweza kula keki hiyo.


 MC. Joshua Makondeko - TutapitaKatikatiYao
 Bahati Bukuku
 Flora Mbasha (kushoto)
 Edson Mwasabwite



 Tumaini Njole

 Mtangazaji wa Sifa Moto Praise Power Radio Judith Njole (kushoto) na Madam Ruti (kulia)

 Mess Jacob Chengula


 Mkate wa Mega Mkate na Praise Power Radio

Watangazaji wa Praise Power Radio Frida (kulia) na Victoria Syaona

BONYEZA "READ MORE" HAPO CHINI KUSHOTO KUONA MATUKIO MENGINE YA EVENT HII YA MEGA MKATE



 Mc. Bony Magupa (Mtangazaji wa Channel 10, na Praise Power Radio)

Flora Mbasha (kushoto) na Bahati Bukuku (kulia)

 Watangazaji wa Praise Power Radio kutoka kulia ni Frida, Hellen, Tina Mtua na Judith Njole
 Mtangazaji wa Praise Power, Veronica Frank


 Kulia ni kaka ambaye alikuwa ameolewa na mzugu lakini sasa ameokoka na amechana tabia ya ushoga. Mungu amebariki maisha yake amepata kazi, anaishi maisha mazuri, ana gari zuri. Aliweza kuwashukuru watangazaji wa Praise Power na Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa kuchangia kuacha tabia ya ushoga
 Kulia ni Mwimbaji wa Gospel kutoka Nigeria Peaceking David
 Veronica Frank aliweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kaka huyu kuachana na ushoga






 Watangazaji wa PPR
 Kasaki Selemani Kikwankwa
 AndrewKihwelo



The Jordan Band walipiga LIVE ngoma za asili
 Kutoka kulia ni MC Joshua makondeko, Mwinjilisti Dunstan, na muwakilishi wa mgeni rasmi wa uzinduzi wa albam ya He Touched Me ya Vocapella Music band

The Jordan Band







  
 






TUNAPOST MATUKIO MENGINE ENDELEA KUTEMBELEA BLOGU YETU

No comments:

Post a Comment

WALIOTEMBELEA - VISITORS

BLOG designer: Rumafrica

BLOG designer: Rumafrica
Blog hii imetegenezwa na Rumafrica +255 715 851 523 | www.rumaafrica.blogspot.com | www.facebook.com/Rulea Sangaa/